Speaker: Caroline

Swahili language wiki ethnologue
Niger–Congo language family wiki
Latin script scriptsource
Roman Catholic Church wiki

Sign of the Cross

Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina

Lord's Prayer

Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani ka mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina

Hail Mary

Salamu, Maria, umejaa neema, Bwana yu nawe, umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na saa ya kufa kwetu. Amina

Gloria Patri

Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu. Kama mwanzo, na siku zote, na milele na milele. Amina