Locuteur: Caroline
Langue Swahili | wiki ethnologue |
Famille des langues Nigéro-congolaise | wiki |
Écriture latin | scriptsource |
Église catholique (romaine) | wiki |
Signe de la Croix
Kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
Notre Père
Baba yetu uliye mbinguni,
jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.
Utakalo lifanyike duniani ka mbinguni.
Utupe leo mkate wetu wa kila siku.
Utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea.
Usitutie katika kishawishi,
lakini utuopoe maovuni.
Amina
Je vous salue Marie
Salamu, Maria, umejaa neema,
Bwana yu nawe,
umebarikiwa kuliko wanawake wote,
na Yesu, mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
Maria mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu,
sasa na saa ya kufa kwetu.
Amina
Gloire au Père
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.
Kama mwanzo, na siku zote, na milele na milele.
Amina