Locuteur: Clarisse
Langue Swahili congolaise | wiki ethnologue |
Famille des langues Nigéro-congolaise | wiki |
Écriture latin | scriptsource |
Église catholique (romaine) | wiki |
Signe de la Croix
Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina
Notre Père
Baba yetu, uliye mbinguni
jina lako litukuzwe.
Ufalme wako ufike.
Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni.
Utupe leo chakula chetu cha kila siku,
utusamehe makosa yetu,
kama tunavyowasamehe waliotukosea.
Usituache kushina vishawishi,
alakini utuopoe katsika Mwovu.
Amina
Je vous salue Marie
Salamu Maria, umejaa nema,
Bwana ni nawe,
mbarikiwa kuliko wanawake wote
mbarikiwa mtote wa tumbo lako Yesu.
Maria mtakatifu,
Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu,
sasa na wataki wa kufa kwetu.
Amina
Gloire au Père
Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.-----
Kama mwanzo, na siku zote, na milele na milele.
Amina
Symbole des Apôtres
Ninamwamini Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia,
Na Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu,
aliyetwaa mwili kwa tendo la Roho Mutakatifu,
akazaliwa na Bikira Maria.
Akateswa zamani za Pontio Pilato,
akasulibiwa, akafa, akazikwa,
akashuka kuzimuni mwa wafu,
akafufuka katika wafu siku ya tatu,
akapanda mbinguni,
anakaa kwa mukono wa kuume wa Mungu,
Baba Mwenyezi,
ndipo atakuja tena kuhukumu wazima na wafu.
Ninamwamini Roho Mutakatifu,
Eklesia katolika takatifu,
ushirika wa watakatifu,
ondoleo la zambi,
ufufuko wa mwili,
na uzima wa milele.
Amina