Mluvčí: Clarisse

Jazyk Svahilština, konžská wiki ethnologue
Nigerokonžská jazyková rodina wiki
latinské písmo scriptsource
Římskokatolická církev wiki

Znamení kříže

Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina

Otčenáš

Baba yetu, uliye mbinguni jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo chakula chetu cha kila siku, utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe waliotukosea. Usituache kushina vishawishi, alakini utuopoe katsika Mwovu. Amina

Zdrávas Maria

Salamu Maria, umejaa nema, Bwana ni nawe, mbarikiwa kuliko wanawake wote mbarikiwa mtote wa tumbo lako Yesu. Maria mtakatifu, Mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu, sasa na wataki wa kufa kwetu. Amina

Sláva Otci

Atukuzwe Baba, na Mwana na Roho Mtakatifu.----- Kama mwanzo, na siku zote, na milele na milele. Amina

Apoštolské vyznání víry

Ninamwamini Mungu, Baba Mwenyezi, Muumba wa mbingu na dunia, Na Yesu Kristo, Mwana wake wa pekee, Bwana wetu, aliyetwaa mwili kwa tendo la Roho Mutakatifu, akazaliwa na Bikira Maria. Akateswa zamani za Pontio Pilato, akasulibiwa, akafa, akazikwa, akashuka kuzimuni mwa wafu, akafufuka katika wafu siku ya tatu, akapanda mbinguni, anakaa kwa mukono wa kuume wa Mungu, Baba Mwenyezi, ndipo atakuja tena kuhukumu wazima na wafu. Ninamwamini Roho Mutakatifu, Eklesia katolika takatifu, ushirika wa watakatifu, ondoleo la zambi, ufufuko wa mwili, na uzima wa milele. Amina